Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia asisitiza uwekezaji katika nishati safi ya kupikia
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia asisitiza uwekezaji katika nishati safi ya kupikia

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameieleza dunia kuwa uwekezaji wa kweli katika nishati ni kuwekeza katika nishati safi ya kupikia barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati anahutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Korea na Afrika unaofanyika Seoul, Korea tarehe 4 na 5 Juni 2024.

Rais Samia amesisitiza umuhimu wa wadau kuongeza ushrikiano ili kuharakisha utekelezaji wa agenda hiyo ambayo sio tu itapunguza tatizo la uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa misitu, bali itapunguza pia vifo vinavyotokana na magaonjwa yanayotokana na matatizo ya upumuaji.

Rais Samia amesema kuwa uwekezaji katika nishati salama barani Afrika utaongeza fursa za kiuchumi kwa kubuni miradi itakayo kuwa ufumbuzi wa kupata nishati safi ya kupikia.

Rais Samia amemalizia kwa kusema kuwa yeye na Rais wa Benki ya Afrika, Dk. Akinwumi Adesina wapo katika zoezi la kutafuta fedha za kutekeleza agenda hiyo na kutoa wito kwa Korea kuunga mkono zoezi hilo.

Mkutano wa Korea-Afrika ni mara ya kwanza kufanyika kwa ngazi ya Wakuu wa Nchi na unajadili maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya Korea na Afrika, kuhamasisha mageuzi ya viwanda na miundombinu ya kidigitali hasa katika sekta ya kilimo na uvuvi na kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazozikabili dunia hasa katika uhaulishaji wa teknolojia ya miradi ya kilimo. (agricultural technology transfer projects).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!