Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia apangua tena Ikulu, amtumbua DED Misungwi
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Rais Samia apangua tena Ikulu, amtumbua DED Misungwi

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi na uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Joseph Constantine Mafuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Nafasi ya Mafuru imechukuliwa na Addo Missama. Kabla ya uteuzi, Missama alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi wengine walioteuliwa ni Dk. Ashura Abdul Katunzi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kabla ya uteuzi, Dkt. Katunzi alikuwa Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Shirika la Viwango Tanzania(TBS). Dk. Katunzi anachukua nafasi ya Dk. Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

Amnemteua Hassan Juma Mnyika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Kabla ya uteuzi, Mnyika alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu. Mnyika anachukua nafasi ya Lain Ephraim Kamendu ambaye amestaafu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!