Sunday , 7 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia aahidi ushirikiano Rais mpya TEC
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia aahidi ushirikiano Rais mpya TEC

Spread the love

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza Serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati Rais mpya wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema wakati wote atakapokuwa na jambo ambalo anadhani Serikali inahitaji kushauriwa awe huru na wakati wote anapoona kwamba anahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, atapewa ushirikiano.

Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake imeshaagiza ushirikiano huo usiwe tu ngazi ya kitaifa bali uende hadi katika ngazi ya vitongoji “Tuendelee kuwa pamoja na kuja kwangu hapa nikuhakikishie tunaendelea kukupa ushirikiano”

Majaliwa amesema hayo wakati akiwasilisha Salamu za Pongezi kutoka kwa Rais Samia leo Jumatano kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi.

Amesema Rais Samia anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

“Tunashukuru tunapata ushauri, yapo mambo ambayo mnayafanya na kuiwezesha nchi hii iendelee, mshikamano wetu ndani ya nchi, umoja wetu ndio unaozaa utulivu na amani tuliyonayo”

Amesema kuwa Serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati “wakati wote utakapokuwa na jambo ambalo unadhani Serikali inahitaji kushauriwa uwe huru na wakati wote unapoona kwamba unahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, sisi tutakupa ushirikiano”

Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake imeshaagiza ushirikiano huo usiwe tu ngazi ya kitaifa bali uende hadi katika ngazi ya vitongoji “Tuendelee kuwa pamoja na kuja kwangu hapa nikuhakikishie tunaendelea kukupa ushirikiano”

Kwa upande wake Askofu Pisa amemshukuru Rais Dk. Samia Kwa salamu za pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa TEC

Uchaguzi wa viongozi wapya wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) uliohusisha nafasi za Rais, Makamu wa Rais na Katibu ulifanyika tarehe Juni 21, mwaka huu, ambao waliochaguliwa ni Mhashamu Wolfgang Pisa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi (Rais), Mhashamu  Eusebius Nzigilwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda (Makamu wa Rais) na Padre Charles Kitima Padre wa Jimbo Katoliki la Singida (Katibu Mkuu).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Spread the loveUamuzi wa Serikali ya Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TAWA yakaribisha Watanzania, wageni kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini

Spread the loveMAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iimetoa wito kwa...

error: Content is protected !!