Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko NGO ya Kapuya yachunguzwa kwa ushoga
Habari MchanganyikoTangulizi

NGO ya Kapuya yachunguzwa kwa ushoga

Spread the love

SERIKALI imeanza kuichunguza Taasisi ya Athuman Kapuya, dhidi ya tuhuma za usambazaji ushoga inazoikabili shirika hilo lisilo la kiserikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya uchunguzi huo imetolewa Leo tarehe 4 Juni 2024 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, ikiwa ni siku Moja tangu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, kuifungia Taasisi hiyo baada ya kudaiwa kusambaza vitabu na bidhaa nyingine zinazotumiwa na watu wanaofanya mapenzi ya Jinsia Moja hususan ushoga.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha akionesha vitabu vinavyohamasisha vitendo vya ndoa za jinsia moja vilivyoingizwa Tabora na taasisi hiyo.

Kupitia taarifa yake, Dk. Gwajima amesema uchunguzi huo unafanyika ili kubaini ukweli wa madai hayo na ikithibitika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa Taasisi husika kwa kosa la kukiuka Sheria, mila na desturi za Tanzania.

“Kutokana na upungufu huo, ofisi ya msajili kupitia bodi ya uratibu wa mashirika hayo imesimamisha utendaji kazi wa shirika hilo kote nchini ili kupisha uchunguzi na hatua zaidi. Baada ya uchunguzi kukamilika wahusika watachukiliwa hatua zote stahiki kwa mujibu wa Sheria,” imesema taarifa ya Dk. Gwajima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!