Friday , 28 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Nape awaomba wadau wa habari wamuamini
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Nape Nnauye
Spread the love

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba wadau wa sekta ya habari kuwa na imani naye kuhusu vifungu 12 vinavyolalamikiwa katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo ya Waziri Nape ilitokana na maazimio sita ambayo yalisomwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba, ambapo moja ya azimio lilikuwa ni vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari ambavyo vinalalamikiwa na wadau wa sekta hiyo.

Nape ametoa kauli hiyo wakati akifunga Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari lilifoanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa siku mbili na kushirikisha wadau zaidi 1,200 kutoka sekta umma na binafsi kwenye tasnia ya habari.

Makoba alitaja maazimio mengi kuwa ni wizara na taasisi za serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari ifikapo Disemba 24 mwaka 2024 na wamiliki waweze kulipa mishahara, pia azimio lingine serikali kuangalia uwezekano wawekezaji wakigeni kuwa na asilimia 75, vyombo vya habari kuandika habari za kijamii, vyombo vya habari vitoe fursa kwa vyama vyote na vyombo vya habari vya mtandao viongoze ubunifu na kuandaa maudhui yenye tija na kujijengea uaminifu kwa walaji.

Amesema amekuwa akisikitishwa na muendelezo wa kulalamikia vifungu 12 vya sheria hiyo, huku akiwa ameelezea kwanini havikufanyiwa mabadiliko wakati wa mabadiliko yaliyohusisha vifungu tisa pekee vya sheria hiyo.

Waziri Nape amesema kuna vifungu ambavyo vinahitaji mabadiliko ya sera ndio viweze kubadilika na vingine vitaingizwa kwenye kanunu, hivyo anawataka wadau kuacha kulalamika wakihisi kwamba serikali haitaki.

“Hili suala la vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari ambavyo mnavitaja kila mara, nadhani nimefafanua sana kwamba hoja hizi tutazifanyia kazi baada ya sera mpya kutungwa na vingine vitaingia kwenye kanuni, najisikia vibaya kwa sababu tumefanya vikao na kukubaliana.

“Nitatoa mfano hoja ya umiliki wa vyombo vya habari, ipo kwenye Sera ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2003, mimi sikuwepo, nilikuwa ndio naanza kazi CCM. Jamani naomba tuaminiane, mimi ni mdau wa sekta hii kwa sababu nimeisomea. Sitengenezi kwa ajili yangu au ajili yenu, ni kwa ajili yetu, kwa sababu sijui watoto wangu watafanya kazi gani. Tuaminiane. Tutafika salama,” amesema.

Waziri Nape amesema katika mchakato huo wa kubadilisha sheria aliwashirikisha baadhi ya waandishi na kuwaonesha hali halisi, hivyo anaumia pale ambapo anatiliwa mashaka katika hilo.

Amesema aliwasilisha sheria bungeni na mjadala ukawa mkali kwa wabunge kutaka mabadiliko na alikubali  mabadiliko ambayo wabunge walitaka, jambo  ambalo halijafanywa na waziri yoyote.

“Sikilizeni mimi naipenda sekta hii, kiasi kwamba 2017 nilikuwa tayari kupoteza uwaziri, kulinda uhuru wa vyombo vya habari wa nchi hii, msisahau rekodi hizi, sekta ya habari ipo ndani ya moyo wangu, siku ile wakina Deudatus Balile, Jesse Kwayu na wengine wanaenda kusoma ripoti nilijua nafukuzwa, waliniambia nitafukuzwa nikawaambia nilipofikia siwezi kurudi nyuma, uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kuliko kazi yangu.

Siwezi kuingi kwenye rikodi ya kuhujumu vyombo vya habari kwa sababu utanifuata maisha yangu yote, kwa sababu ya cheo tu. Si nilitoka leo nimerudi nasonga mbele na heshima yangu ipo, wanahabari msisahu, sekta ya habari ipo mikono salama. Na wao wanajua, wasioitakia mema sekta hii wanajua, ilimradi Nape yupo atasimamia na wanahabari wake,” amesema.

Nape amewahakikishia wadau wa sekta ya habari kuwa serikali chini ya uongozi Rais Samia Suluhu Hassana ina dhamira ya kweli ya kujenga ushirikiano, ili kuhakikisha kila upande unanufaika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the loveRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watanzania waonywa kutotumia uchaguzi kuvuna hela

Spread the loveWATANZANIA wametakiwa kutotumia uchaguzi kuwa wakati wa mavuno ya pesa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Spread the loveWakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa gesi yaja na mitungi ya bei nafuu kwa wanafunzi vyuo vikuu

Spread the loveKampuni ya kuuza nishati ya gesi ya kupikia majumbani ya...

error: Content is protected !!