Friday , 28 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake
Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the love

Hali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti ya Nandi nchini Kenya baada ya Ofisa wa Jeshi la nchini hiyo (KDF) kudaiwa kumuua kasisi wa kanisa la Angalikan (ACK) kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni fumanizi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, Ofisa huyo alirejea nyumbani kinyemela nyakati za usiku na kumfumania mtumishi wa Mungu, James Kemei mwenye umri wa miaka 43 kwenye kitanda chake na mke wake wakishiriki mapenzi kabla ya kumchoma kwa misumari kwenye uti wa mgongo na kumkata uume wake.

Afisa huyo anadaiwa kudokezwa kuhusu mkewe na kasisi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi kisha akamvizia nyumbani kwake na kuingia katika chumba kimoja bila ya mkewe kujua.

Inasemekana alisubiri kwa hadi saa mbili asubuhi ili wawili hao kwaingie kitandani  ndipo alipowafumania  na kuanza kumshambulia kwa adhabu kali mgoni wake hali iliyosababisha umauti wake akiwa hospitalini.

Aidha, Ofisa huyo anadaiwa alimgeukia mke wake, na kumvunja mkono ilihali mgoni wake akimpigilia misumari kwenye uti wa mgongo.

Majirani waliambia gazeti la The Star kuwa afisa huyo alimweka mke kwenye kona ya chumba cha kulala huku akimchinja mpenzi wake kwa kumkata sehemu zake za siri huku mkewe akishuhudia.

Kamanda wa polisi wa Nandi, Dickens Njogu alisema mtoa taarifa ambaye jina lake halikufahamika, aliwapigia simu polisi kuhusu tukio hilo muda wa saa tatu asubuhi jana Alhamisi.

“Ilikuwa tu asubuhi ya leo (jana) wakati Mkuu wa Kanisa Kuu la St Barnabas, Mchungaji Nillah Bassy alipokuja kutoa ripoti rasmi ya tukio hilo la kusikitisha ambalo maafisa wa polisi walienda kulifuatilia,” afisa huyo alisema.

Majirani walimkimbiza Mchungaji Kemei katika hospitali ya Kapsabet Level 5 akiwa katika hali mahututi. Alihamishiwa huko Eldoret ambapo walitangaza kuwa amefariki alipofika katika Hospitali ya Top Hill.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the loveRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watanzania waonywa kutotumia uchaguzi kuvuna hela

Spread the loveWATANZANIA wametakiwa kutotumia uchaguzi kuwa wakati wa mavuno ya pesa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Spread the loveWakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa gesi yaja na mitungi ya bei nafuu kwa wanafunzi vyuo vikuu

Spread the loveKampuni ya kuuza nishati ya gesi ya kupikia majumbani ya...

error: Content is protected !!