Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Sultan Saleh Seif
Spread the love

Wakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif, ameruhusu wananchi kuendea la shughuli hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Seif alitoa kauli hiyo jana (June 26, 2024) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ninde, Kata ya Ninde wilayani Nkasi mkoani humo.

Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, akitangaza lengo la Serikali la kufunga kwa muda shughuli za uvuvi alisema lengo ni kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli zao ziwani humo.

Kauli za Seif zilizonukuliwa katika video fupi inayozunguka mitandaoni, ikimnukuu MNEC huyo akihamasisha wananchi kuendea na shughuli za uvuvi, inatofautiana na sababu zilizotolewa na Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdala Ulega ambaye alisema uamuzi wa Tanzania unatokana makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ulega alisema uamuzi huo ni utekelezaji wa Mkataba wa Kikanda wa Nchi Wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaoweka hatua na taratibu za usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.

Aliongeza uamuzi huo unatokana na utafiti uliobainisha kuwa kumekuwepo na upungufu mkubwa wa samaki na dagaa katika ziwa Tanganyika kunakotokana na ongezeko kubwa la uvuvi usio endelevu uliopelekea uharibifu wa mazalia ya samaki.

https://x.com/Mwanahalisitz/status/1806327549976256887

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!