Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko INEC yawanoa wasimamizi wa vituo vya uchaguzi jimbo la Kwahani
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

INEC yawanoa wasimamizi wa vituo vya uchaguzi jimbo la Kwahani

Spread the love

Wasimamizi wakuu na wasaidizi wa vituo vya Kupiga kura katika jimbo la Kwahani mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wametakiwa kufanya kazi kwa kujiamini, uadilifu na weledi wanapotekeleza majukumu yao ya uchaguzi kutokana na dhamana waliyopewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Zakia Mohamed Abubakar wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yanayofanyika kuanzia leo tarehe 5 hadi 6 Juni, 2024 Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi- Zanzibar.

“Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu ya imani ya Tume kuwa mnao uwezo wa kufanya kazi hii, jambo muhimu mnalotakiwa kulizingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yenu mnapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume,”alisema Dk. Zakia.

Dk. Zakia amesema, kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hii ni pamoja na Chaguzi ndogo zinazojitokeza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vifo kama ilivyotokea katika Jimbo la Kwahani.

“Hata hivyo, pamoja na kuwa Tume ndiyo yenye jukumu hilo, wanaoratibu na kusimamia Uchaguzi ngazi ya Vituo ni nyinyi tuliowateua pamoja na watendaji wengine”.

Aidha, Dk. Zakia amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa Uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama siyo kuondosha kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi.

Amewataka washiriki hao wa mafunzo kuwa watulivu na kupokea mada zitakazowasilishwa, wabadilishane uzoefu na kujadili namna ya kufanikisha Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani.

“Nachukua fursa hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katikauendeshaji wa Uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Dk. Zakia.

Aidha, amewataka kuhakiki vifaa watakavyovipokea kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kuhakikisha kila Msimamizi wa Kituo anapata vifaa vyote vya Uchaguzi vinavyohitajika mapema.

Pia, Dk. Zakia amewasisitiza kuwa siku ya Uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha Kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi; na kufanya mawasiliano na Msimamizi wa Uchaguzi pale ambapo utahitajika ushauri kuhusiana na masuala ya Uchaguzi uliopo.

Kabla ya kufungua Mafunzo hayo, wasimamizi hao na wasimamizi wasaidizi hao walikula kiapo cha kutunza Siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Safia Iddi Muhammad.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza siku ya Jumamosi ya tarehe 8 Juni 2024 kuwa ni siku ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kwahani. Vyama 14 vya siasa vimejitokeza na vinaendelea na kampeni kuelekea siku ya uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!