Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the love

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas kwa kujenga  bohari ya kwanza ya kuhifadhi nishati za gesi huku akizitaka kampuni za gesi kuhakikisha wanaweka mikakati itakayowezesha kupungua kwa bei ya gesi ili waipate kwa gharama nafuu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza  mbele ya wananchi wa Zanzibar baada ya kuzindua bohari hiyo ya kupokea na kuhifadhi gesi pamoja na miundombinu mingine jumuishi, Dk. Mwinyi amepongeza ujenzi wa bohari hiyo huku akizipongeza taasisi nyingine ambazo zimefanikisha ujenzi wa mindombinu jumuishi ya bandari ya Mangapwani ambayo itahusika na meli za mafuta na gesi pamoja na shughuli nyingine.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi wa Kampuni ya Oryx, Joseph Soka alipokuwa akitoa maelezo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bohari ya kuhifadhi nishati za gesi ya kuhifadhi nishati ya gesi ya Kampuni ya Oryx na Vigor Group og Companies uliofanyika jana Juni 27, 2024 Mangapwani Zanzibar.

“Kwa muda mrefu tulikuwa tunamia bandari ya Malindi lakini kutokana na ongezeko la shughuli za kiuchumi bandari ile haitoshi, hivyo Serikali ilitangaza eneo la Mangapwani kuwa bandari kwa ajili ya nishati ya gesi, mafuta na miundombinu mengine.

“Sasa tutakuwa tunapokea meli kubwa na kuhifadhiwa katika  matanki mawili makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi tani 130 yaliyojengwa na Oryx. Hivyo niziombe kampuni nyingine kufuata nyayo za Oryx kwa kujenga miundombinu yao katika eneo hili,”alisema.

Pia alisema kuanzishwa kwa bohari ya kuhifadhi ya gesi Zanzibar kutaongeza chachu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi na hivyo kufikia malengo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwamba ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi ya kupikia huku akisisitiza umuhmu wa bei ya gesi kupunguzwa ili wananchi wengi watumie.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Limited, Benoît Araman alisema kufunguliwa kwa bohari ya gesi Mangapwani inanaonyesha dhamira ya Oryx Energies ya kuwekeza katika miundombinu muhimu inayosaidia matumizi salama na mapana ya gesi ya LPG nchini Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akikata utepe kuweka jiwe la msingi kuzindua bohari ya kuhifadhi nishati ya gesi ya Kampuni ya Oryx uliofanyika jana Juni 27, 2024 huko Mangapwani Zanzibar.

Pia inakidhi ombi la Serikali la kuhakikisha usambazaji endelevu wa LPG kila mahali nchini.Soko la gesi la Tanzania limeshuhudia ongezeko la uagizaji wa bidhaa kutoka nje kwa karibu mara 13 katika muongo uliopita, kutoka tani 20,000 mwaka 2010 hadi tani 293,000 mwaka 2023.

Aliongeza Oryx Gas Zanzibar imeungana na kampuni ya TP Limited yenye makao yake Zanzibar ambayo ni  kampuni tanzu ya Vigor Turky’s Group of Companies (Vigor Group), kujenga bohari hiyo ya kimkakati  na kuongeza usambazaji wa gesi ya LPG kisiwani humo.

“Mkataba huu unaonyesha kujitolea kwa Oryx Energies katika kuendeleza ushirikiano na makampuni ya wazawa.Bohari ya Mangapwani, ambayo ilianza kufanya kazi mapema Mei ina uwezo wa kuhifadhi tani 1,300 za gesi ya LPG, na ilipokea meli yake ya kwanza ya tani 1,200  mnamo Mei 2, 2024.

“Pia kusaidia Mpango wa matumizi wa nishati safi ya kupikia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Gesi ya LPG inazidi kuwa sehemu muhimu ya mchanganyiko wa matumizi ya nishati mbalimbali za kupikia Zanzibar, ikishughulikia mahitaji ya kaya, biashara, na sekta ya utalii inayokua kwa kasi,”alisema.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Zanzibar Limited, Shuwekha Omar Khamis alisema: “Tunajivunia kuzindua bohari hii ya kisasa ya LPG ambalo itaimarisha usambazaji  wa gesi ya LPG katika visiwa hivyo. Tumedhamiria kuendelea kuchukua jukumu muhimu katika maendeleo haya, kwa kuwa tumeweka msingi wa kupanua usambazaji wa LPG Zanzibar.

Awali Mwenyekiti wa kampuni za Vigor Toufiq Salim Turky alisema wameungana Oryx kwasababu ya kutambua uwezo wao  wa miaka mingi katika soko la gesi nchini , hivyo ni imani yao sasa gesi itapatikana kwa wengi.

Pia alisema mpango wao ni kupunguza bei ya gesi Zanzibar kwa asilimia 20 kuanzia Julai 1 mwaka huu na baadae kupungua bei kwa asilimia 30. “Hivyo Oryx Gas wameiweka bohari hii katika viwango vya kimataifa, tunafahamu wao wako kwa miaka mingi, wana uzoefu mkubwa.

“Bohari hii inamilikiwa na Vigor kwa asilimia 100, lakini kwa uendeshaji tumamua kuwapa wenzetu wa Oryx .Uendeshaji tumeukabidhi kwa Oryx kwa kuamini wao ni kinara katika soko la Tanzania.Wakati tunaanza huko nyuma soko lilikuwa ni tani tatu lakini sasa soko lao limekuwa na kufikia tani 800,”alisema.

Kwa upande wake wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA), Omar Ali Yussuf alisema kwa miaka mingi sekta ya nishati hasa gesi, walikuwa wanatumia bandari ya malindi lakini sasa wamepeta bandari ambayo itashusha gesi, mafuta na itatumika kwa shughuli nyingine kwenye hilo la Mangapwani.

“Kabla ya kuwepo kwa bandari hii ya kushusha gesi na mafuta tulikuwa tunatumia majahazi n vingine ambavyo havina salama lakini kwa maelekezo ya Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi leo tumeweza kuwa na bandari kwa ajili ya meli zenye gesi na mafuta,”alisema.

Pia alisema kwa kupitia mipango ya Serikali pamoja na sera nzuri za uchumi wa bluu watahakikisha bandari ya Mangapwani wanataka iwe kituo kikuu cha kusafirisha gesi na mafuta kwa ukanda wa Afrika Mashariki huku akifafanua kuwa bei ya nishati ya mafuta na gesi kwa Zanzibar iko chini ukilinganisha nchi nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!