Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko DAWASA yapeleka matumaini mapya Msumi
Habari Mchanganyiko

DAWASA yapeleka matumaini mapya Msumi

Spread the love

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza  kutekeleza kazi ya uchimbaji visima katika eneo la Mbezi- Msumi Kata ya Mbezi ikiwa ni maagizo ya Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew katika ziara yake aliyoifanya mkoan Dar es salaam katika Wilaya ya Ubungo hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika ziara hiyo, Kundo aliwaeleza wananchi wa Msumi kuwa Serikali kupitia DAWASA imeandaa mkakati wa muda mrefu ambapo  kwa kutenga kiasi cha Sh 18 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa tenki kubwa na ulazaji wa mabomba.

Amesema mkakati wa muda mfupi ni wa kuchimba visima virefu ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa majisafi kwenye eneo hilo lenye wakazi takribani 144,000.

Akizungumza utekelezaji wa maagizo hayo,  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro amesema hatua hii ni ya mwanzo ya kuhakikisha eneo la Msumi linapata huduma  kwani hapo awali eneo hilo halikuwa na mtandao wa maji kutoka DAWASA na hivyo wananchi kutegemea maji kutoka kwenye visima vya watoa huduma binafsi.

“Tupo hapa kujionea utekelezaji wa mkakati wa muda mfupi wa uchimbaji wa visima ambayo vitaenda kupunguza makali ya adha ya ukosefu wa maji katika eneo hili.

“Utofauti wa  visima hivi tunavyochimba DAWASA na vile vya Wananchi ni kuwa visima vyetu ni vyenye urefu  kuanzia mita 170 kwenda chini na utaenda sambamba na ujenzi wa vizimba kwenye mitaa ili kusogeza huduma kwa wananchi.” amesema Lyaro

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Msumi, Ismail Mbinda ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona hali ya eneo la Msumi na  kutatua changamoto hii iliyodumu kwa mda mrefu.

“Kwa kweli tutakua wachoyo wa fadhila kama tusiposhukuru kwa hili, Serikali yetu tunaishukuru sana jitihada zinaonekana na hawa watu wa DAWASA wametupa ushirikiano mno tunaomba hili zoezi likamilike kwa muda ili watu wapate maji tukisubiri mradi mkubwa” amesema Mwenyekiti Mbinda

Naye, Mkazi wa Msumi Center, Nasma Abdallah amesema wanaishukuru Serikali na DAWASA kwa jitihada hizi kwani ukosefu wa maji ulisababisha  kutumia muda mrefu  na kwenda umbali mrefu kutafuta huduma ya maji ambayo bado hayakuwa salama na ya kutosheleza.

Utekelezaji wa mikakati ya kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika eneo la Msumi ni moja ya malengo ya Mamlaka ya kufikisha huduma kwa  wote ifikapo 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!