Friday , 28 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Chalamila achimba mkwara mzito Kariakoo, aapa kuwaonesha ‘show’
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Chalamila achimba mkwara mzito Kariakoo, aapa kuwaonesha ‘show’

Spread the love

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewathibitishia wafanyabiashara waliofungua maduka leo Jumatatu licha ya kuwepo kwa mgomo kwa baadhi yao, kwamba atakayejaribu kuwafanyia vurugu atamuonesha ‘show’. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

“Yule atakayemletea mkwara aliyekubali kufungua, naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonyesha ‘show’ nzima. Kwa sababu mtu anakubali kufungua na wewe unamchimba mkwara, mimi ntakuchimba mkwara na hautainuka tena,” amesema.

Akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao leo Jumatatu, Chalamila amesema pamoja na uwepo kwa mgomo wa baadhi ya wafanyabishara, atalinda biashara zao na hawatafanyiwa vurugu.

RC Chalamila

Pamoja na mambo mengine, Chalamila amesema kero zilizopelekwa na wafanyabiashara hao serikalini zinaendelea kushughulikiwa.

Naye Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amelieleza Bunge kwamba tayari kamati ya wafanyabiashara hao inakutana na serikali hivyo, wabunge waliotaka kauli ya serikali kuhusu sakata hilo akiwamo Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) kuwa wawe na subira.

Wafanyabiashara hao wamegoma kuishinikiza Serikali kutatua changamoto zinazowakabili, ikiwemo kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mgomo huo umeibuka baada ya juzi Jumamosi kusambaa vipeperushi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa mgomo huo utakaoanza leo.

1 Comment

  • Hivi tukijiuliza tatizo ni nini hapo karihakoo? Utendaji, ufahamu, uelewa..! Kutoelewana au joto ya uchanguzi ujao?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko: Tamaduni za kigeni chanzo ukatili wa kijinsia, mauji albino

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu, Dk. Dotto Biteko amesema vitendo vya mmomonyoko...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the loveRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watanzania waonywa kutotumia uchaguzi kuvuna hela

Spread the loveWATANZANIA wametakiwa kutotumia uchaguzi kuwa wakati wa mavuno ya pesa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Spread the loveWakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika...

error: Content is protected !!