Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM yaivaa Chadema
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yaivaa Chadema

Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekituhymu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kutumia mikutano ya hadhara kutoa hotuba za kuchochea vurugu na umwagaji damu katika chaguzi zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Tuhuma hizo zimetolewa Leo Alhamisi na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Emanuel Nchimbi, kwenye ziara yake mkoani Kilimanjaro.

“Wanawaambia waanze kujiandaa na visu na mapanga kwa ajili ya uchaguzi ujao na anasema matumizi yake hayatakuwa kama matumizi tuliyozoea, hatua Moja huanzisha nyingine.

Watu ambao wanatamani nchi yetu imwage damu fahamu wanaanza kidogokidogo kutengeneza mazingira ya kuuwa,” amesema Balozi Nchimbi na kuongeza:

“Mkipna kawaida mtu anayetamka mauaji azomewe paleplale ajue wananchi hawtaaki kuuwana.”

Baada ya Balozi Nchimbi kutoa tuhuma hizo, kada wa Chadema, Patrick Olesosopi akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu, alisema CCM hakijibu hoja za wananchi wanazoibua badala yake  wanajibu masuala ya uchaguzi.

“Wanashindwa mujibu hoja wanajibu vohoja, wanashindwa mujibu kwa Nini mazao hayana solo wanabeba hoja ndogo badala ya kujibi hoja za msingi za watanzania, wanajibu mkutano wa Chadema hawazungumzii maisha yeni wanajibu mapanga,” alisema Sosopi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Msange mkoani Singida, Lissu alisema watamalizana mapema na wasimamizi wa uchaguzi watakaokiuka Sheria ikiwemo kuengua wagombea kiholela.

“Mwaka huu tunaingia kwenye uchaguzi, tunawaambia mapema wakiengua wagombea Wetu wanatutafuta maneno ni lazima tumalizane nao mapema,” alisema Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!