Friday , 28 June 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM Igunga wanolewa kuhusu sheria usalama barabarani
Habari Mchanganyiko

CCM Igunga wanolewa kuhusu sheria usalama barabarani

Spread the love

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Igunga mkoani Tabora, waliogawiwa pikipiki kwa ajili ya shughuli za chama wilayani humo, wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili waepuke ajali za barabarani. Anaripoti Victor Makinda, Tabora … (endelea).

Hayo yameelezwa mjini Igunga na Askari wa  kikosi cha usalama barabarani, Koplo Josiah, wakati akitoa mafunzo ya usalama barabarani yaliyowahusisha wenyeviti, makatibu  wa CCM  wa Jumuiya zote za chama ngazi ya kata jimbo la uchaguzi Igunga.

Koplo Josiah aliwaeleza viongozi hao wa CCM kuzingatia sheria za usalama pindi wanapoendesha vyombo hivyo ili waweze kuepuka  kufanya makosa yatakayowasababishia ajali.

“Kujua tu kuendesha  chombo cha moto haitoshi, mnapaswa kuzijua na kuzifuata sheria zote za usalama barabarani ili muweze kuepuakana na ajali,” amesema Koplo Josiah.

Ameongeza kuwa kila mtu anayetumia chombo cha moto cha usafiri, anapaswa kuwa na leseni hai ya udereva na kuhakikisha kuwa chombo anachokitumia kimekatiwa bima.

Pia amewataka viongozi hao wa CCM ambao hawana leseni za udereva kuhudhuria mafunzo maalum ya udereva kwenye vyuo vya ufundi stadi (VETA).

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mbunge wa Igunga, Nicholaus Ngassa ambaye ndiye aliyeandaa mafunzo hayo kwa viongozi hao wa chama,  amesema kuwa jumla ya pikipiki 64 zimetolewa na CCM kwa viongozi wa kata 16 jimboni Igunga ili waweze kutekeleza majukumu yao..

Ngassa aliwaasa viongozi hao kuhakikisha kuwa wanafuata sheria za usalama barabarani ili waweze kuendesha kwa usalama na kutekeleza majukumu yao ya ujenzi na uenezi wa chama.

Naye mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Igunga, Mafunda Temanywa, amewataka viongozi hao kuzitunza pikipiki hizo ili ziweze kuleta tija iliyokusudiwa.

“Chama kimewapa pikipiki, na leo mnafundishwa sheria za usalama barabarani, zitumieni pikipiki hizo kwa umakini na kufuata sheria za usalama barabarani ili tija iliyokusudiwa ya kuendelea kukijenga chama chetu CCM itimie,“ amesema Mafunda.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Katibu kata wa CCM kata ya Mwamashimba, Jonas Mondi, alimshukuru mbunge huyo kwa kuwaandalia mafunzo hayo ya usalama barabarani na kuahidi kuwa watazifuata sheria zote walizofundishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Mwinyi aipa tano Oryx kwa ujenzi wa bohari ya kuhifadhia gesi Znz

Spread the loveRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watanzania waonywa kutotumia uchaguzi kuvuna hela

Spread the loveWATANZANIA wametakiwa kutotumia uchaguzi kuwa wakati wa mavuno ya pesa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Spread the loveWakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Taifa gesi yaja na mitungi ya bei nafuu kwa wanafunzi vyuo vikuu

Spread the loveKampuni ya kuuza nishati ya gesi ya kupikia majumbani ya...

error: Content is protected !!