Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Baba amuua kinyama mtoto wake, anyofoa sehemu za siri
Habari Mchanganyiko

Baba amuua kinyama mtoto wake, anyofoa sehemu za siri

RPC Alex Mkama
Spread the love

ERICK Magulu (33), mkazi wa wilaya ya Kilombero, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, kwa tuhuma za kumuua kinyama mtoto wake wa kambo, Johnson Mgongano (6). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 4 Juni 2024, Kamanda wa Jeshi la Polisi Morogoro, Alex Mkama, amedai mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo tarehe 1 Juni 2024.

Kamanda Mkama amedai kuwa, Magulu alimuua mwanawe kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili, kisha akanyofoa sehemu zake za Siri.

Amesema baada ya mtuhumiwa kukamata kufuatia taarifa za raia wema, alihojiwa na kukiri kutekeleza tukio hilo Kisha kuonesha mahali vilipo viungo hivyo.

“Magulu alimchinja mtoto akatenganisha kichwa na viungo vingine vya mkono na sehemu za siri. Mtuhumiwa alikamatwa alihojiwa na kukiri kufanya mauaji hayo na kutoa ushirikiano kuonyesha sehemu aliyoweks viungo na vilipatikana,” amesema Kamanda Mkama.

Kamanda Mkama amesema viungo vinavyodaiwa kuwa vya Ngonyani vitafanyiwa uchunguzi wa kisayansi, Kisha taratibu nyingine za kisheria zitafuatwa.

Katika tukio lingine, Kamanda Mkama amesema wanashikilia Jovi Steven, kwa tuhuma za kula njama za kumuuwa mume wake Christian Revocatus, huku chanzo kikiwa na mgogoro wa muda mrefu wa ndoa.

“Revocatus aliuawa kwa kupigwa na kitu butu akiwa amelala na mke wake, upelelezi unaendelea kukamata watuhumiwa wengine walioshirikiana na huyo mama. Chanzo cha mauaji wamekuwa na changamoto ya mgogoro kwenye ndoa yao katika kipindi chote walichoishi,” amesema Kamanda Mkama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!