Sunday , 7 July 2024
Home Habari Mchanganyiko CAG atoa kongole kwa PPAA
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CAG atoa kongole kwa PPAA

Spread the love

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kichere ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la PPAA katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Agnes Sayi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando amemueleza CAG kuwa Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 imeboresha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja kupunguzwa kwa muda wa kushughulikia malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma kutoka siku 45 hadi siku 40.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Agnes Sayi wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

“Mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwa lengo la kupunguza muda, kuongeza uwazi na usawa katika shughuli za ununuzi wa umma, kuongeza ushindani,” alisema Sayi

Kadhalika Sayi ameongeza kuwa PPAA imefanikiwa kuanzisha Moduli ya kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia kieletroniki ambapo moduli hiyo ipo katika mfumo wa ununuzi wa umma kieletroniki (NeST) ambapo kupitia moduli hiyo wazabuni wataawasilisha malalamiko yao kieletroniki jambo ambalo litasaidia kuokoa muda na gharama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Spread the loveUamuzi wa Serikali ya Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TAWA yakaribisha Watanzania, wageni kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini

Spread the loveMAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iimetoa wito kwa...

error: Content is protected !!