MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Morogoro inatarajia kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara 27 kwa kutozingatia matumizi ya mashine za Kielektroniki (EFD). Anaripoti Christina Cosmas, Morogoro … (endele).
Meneja wa TRA mkoani hapa Sylver Rutagwelera alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na wanaokataa kutoa risiti za EFD kwa wateja, wanaojaribu kuwatoza wanunuzi fedha za ziada ili wawapatie risiti za kielektroniki na wanaodaiwa madeni ya muda mrefu.
Rutagwelera alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na wenye maduka ya nguo, vyombo vya ndani na bidhaa zingine ambao wamefuatiliwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2022/24 ambapo zoezi hilo ni endelevu.
Alisema tayari kesi tisa zimeshaingia katika mfumo wa mahakama na zingine zitaingizwa na kufikia 27 na kwamba 21 ni kwa ajili ya kukiuka matumizi ya EFD, kutolipa adhabu wanazopewa, wanaandikiwa barua hawajiri.
Leave a comment