Sunday , 7 July 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Msumbiji kutua nchini leo, Samia kumpokea kesho
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Msumbiji kutua nchini leo, Samia kumpokea kesho

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi kesho tarehe 2 Julai 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonyesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga imesema Rais Nyusi anatarajiwa kuwasili nchini leo Jumatatu jioni ambapo atafanya ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Imesema Rais Samia na mgeni wake Rais Nyusi watashiriki mazungumzo ya pamoja ambayo yatajikita katika sekta ya biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama na kisha kushuhudia uwekaji saini wa makubaliano katika sekta mbalimbali za ushirikiano.

“Ziara hii itaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria, kidugu na kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ambao uliasisiwa na viongozi wetu; kiongozi wa kwanza wa chama tawala cha nchi hiyo (FRELIMO), Hayati Eduardo Chivambo Mondlane na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere.

“Rais Nyusi pia anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) siku ya tarehe 3 Julai 2024 ambapo ataambatana na mwenyeji wake Rais Samia.

Rais Nyusi ataondoka nchini tarehe 4 Julai 2024,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali yakanusha kuchelewa kutoa vibali vya uagizaji wa sukari

Spread the loveBODI ya Sukari Tanzania imekanusha taarifa za kuchelewa kutoa vibali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Uamuzi wa serikali kuwapa wafanyabiashara vibali vya uagizaji kulishusha bei ya sukari

Spread the loveUamuzi wa Serikali ya Tanzania kutoa vibali vya uagizaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TAWA yakaribisha Watanzania, wageni kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini

Spread the loveMAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iimetoa wito kwa...

error: Content is protected !!