Wazazi na walezi Kijiji cha Ipapa Kata ya Ipunga Wilaya ya Mbozi mkoni Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwafanya watoto vitega uchumi vya kuendesha familia na kuwakoseha haki yao ya msingi ya kupata elimu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).
Wito huo umetolewa jana Jumanne na Polisi Kata ya Ipunga, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eletisia Mtweve alipokuwa anatoa elimu ya madhara ya ajira kwa watoto aliowakuta kijijini hapo wakifanyishwa kazi za kiuchumi ili kuendesha familia zao.
“Ajira kwa watoto inaonesha unyonyaji kwa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima kuishi kwenye utoto wao, inawafanya washindwe kuhudhuria shule na inawaletea madhara ya kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili” alisema Mkaguzi Mtweve
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu katika jamii kwa kuyafikia makundi mbalimbali na kuwajengea uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu usalama ili jamii iache matendo maovu na kuuchukia uhalifu kwa usalama wa mali zao.
Leave a comment