Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanunuzi wa madini Songwe wampa tano Samia kupaisha sekta ya madini
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wanunuzi wa madini Songwe wampa tano Samia kupaisha sekta ya madini

Spread the love

WANUNUZI wa madini ya dhahabu mkoani Songwe wamempongeza Rais Samia SuluhuHassan kwa kufanya mapinduzi ya kiuchumi katika sekta hiyo kwa kuiwezesha kupaa maradufu kimapato ikilinganishwa na miaka iliyopita. Anaripoti Ibrahim Yaasin, Songwe… (endelea).

Wakizungumza na MwanaHALISI jana Jumatano katika ofisi za madini zilizopo Mkwajuni wilayani Songwe, Mkurugenzi wa kampuni ya ununuzi wa madini, Mohammed Sharif amesema jitihada za Rais Samia pia zimewezesha kuzuia utoroshwaji wa madini.

Amesema awali walikuwa wakiwafuata wachimaji majumbani mwao kuomba wawauzie dhahabu huku wengine wakigoma wakitaka kusafirisha nje ya mkoa hali hiyo iliyowapa ugumu kupata mzigo na kuhatarisha usalama wao na fedha zao kutokana na ulinzi mdogo.

Amesema baada ya ujenzi wa soko la pamoja na kuweka bei elekezi kwenye mbao za matangazo, wamenunua dhahabu kwa urahisi na hata wachimbaji wamekuwa wakipeleka kuuza madini yao katika soko hilo hali iliyomaliza utoroshwaji wa dhahabu.

Ameongeza kutokana na mageuzi hayo, wameweza kusaidia jamii inayozunguka soko hilo katika nyanja mbalimbali ikiwamo sekta za afya, elimu, umeme, miundombinu ya barabara na kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada ikiwemo misikiti.

Mbali na kusaidia jamii hususani kwenye ujenzi, Sharif pia amesema wamewajengea nyumba mbili wazee wasiojiweza ambazo zipo asilimia 80 za ujenzi pamoja na kutoa michango mbalimbali katika halmashauri.

Naye Said Mabruki ambaye pia ni mnunuzi wa madini, amesema kutokana na uwepo wa soko hilo la pamoja, wametoa ajira zaidi ya 60 katika kada mbalimbali kwa vijana wanaojishughulisha na uchimbaji kwa kuwapa mitaji.

Naye Mnunuzi wa madini, Fove Swaleh amesema siku za hivi karibuni Rais Samia kupitia waziri wa madini Anthony Mavunde, alitoa leseni za vitalu 19 kwa vikundi vya wachimbaji hali itakayowasaidia kukopesheka kwa kuwa watakuwa na leseni ambazo ni kama dhamana kwao.

Kwa upande wake Chonde Malembo amesema katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia hali ya kipato kwa wadau wa sekta ya madini kimeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Kwa sababu madini yote yanauzwa kwa bei elekezi ambayo kwa gram 1 inauzwa Sh 176,000 na wanunuzi wote wapo sehemu moja ambayo inarahisisha hata serikali kuchukua mapato yake. Pia hakuna utoroshwaji wa madini na hadi kufikia Mei mwaka huu walikusanya asilimia 71 za mapato,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!