MADEREVA wawanaosafirirsha abiria kwa kutumia pikipiki (bodaboda), wametakiwa kuendelea kufanya shughuli zao kwa umakini kwa kuwa kazi hiyo ndiyo inayowapa riziki ya kuendesha maisha yao na familia zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo umetolewa leo Jumatano na Mwanaharakati Bihimba Mpaya, wakati anakibidhi msaada wa pikipiki tatu kwenye kikundi cha Bodaboda Kivule, kilichopo jijini Dar es Salaam.
Bihimba ambaye ni mlezi wa kikundi hicho, amesema kuna baadhi ya bodaboda wamefanikiwa kujenga nyumba na kujikwamua kiuchumi kupitia kazi hiyo.
“Leo nikiongea na vijana wangu nilichowaambia wafanye kazi kwa bidii na kwa kifua mbele kwa kuwa ni bodaboda ni kazi kama zilivyo kazi zingine ndio maana vijana wameweza kupanga vyumba vya kuishi na familia zao Hadi wengine wamenunua viwanja na wanaanza kujenga,” amesema Bihimba.
Bihimba amesema ametoa msaada wa pikipiki hizo ili kuwasaidia vijana wengine wasiokuwa nazo waweze kujiajiri.
Leave a comment