Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Baba mzazi, mganga, paroko wadakwa mauaji ya mtoto mwenye ualbino
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Baba mzazi, mganga, paroko wadakwa mauaji ya mtoto mwenye ualbino

Spread the love

HATIMAYE Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya mtoto Asimwe Novart mwenye ualbino, wakiwa wamevihifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta mteja. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.

Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP-David Misime amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.

Amesema Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo.

Pia ameonya waache kudanganyana kwamba kuna utajiri unaopatikana kwa kumiliki viungo vya binadamu mwenye ualbino kwani si kweli kwasababu kama ingekuwa hivyo familia zenye watoto au ndugu wenye ualbino wangekuwa na utajiri mkubwa lakini badala yake tunaona wakishi maisha ya kawaida kama sisi wengine.

“Vitendo hivyo wakumbuke ni uhalifu uliopitiliza, ni ushamba katika karne hii ya maendeleo ya sayansi na teknolojja kwani yeyote yule anayefanya na anayeshiriki katika uhalifu wa aina hiyo lazima atakamatwa kwa sababu vitendo hivyo havina baraka za mwenyezi Mungu wala za sheria za nchi.

“Ni vitendo vya aibu kwa anayefanya, kwa familia yake na pia wanalifedhehesha taifa. Watu wenye mawazo hayo waachane nayo wafanye kazi halali, watoke jasho na ndiyo siri ya kufanikiwa katika maisha na siyo kuendekeza ushirikina na kupiga ramli chonganishi,” amesema Misime.

Ikumbukwe kuwa tarehe 30 Mei 2024 majira ya saa mbili usiku huko katika kiji cha Bulamula Wilaya ya Muleba mkoani Kagera kulitokea tukio la kusikitisha na la kulaaniwa ambapo mtoto aitwaye Asimwe Novart mwenye umri wa miaka miwili na nusu mwenye ualbino aliporwa na watu wasiofahamika kutoka kwa mama yake mzazi.

Tarehe 17 Juni 2024 majira ya saa sita mchana mtoto huyo alipatikana akiwa ameuawa kikatili kwa kukatwa baadhi ya viungo vyake na kufungwa kwenye mfuko kisha kutupwa kwenye kalavati linalopitisha maji katika barabara itokayo Luhanga kwenda katika kiji cha Makongora.

Baada ya tukio hilo kutokea, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wadau wengine walilaani tukio hilo huku Jeshi la Polisi likiahidi kuwakamata watuhumowa hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!