Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaahidi kushirikiana na UNCDF, EU kusaidia ajenda nishati safi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na UNCDF, EU kusaidia ajenda nishati safi

Spread the love

Imeelezwa kuwa, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na washirika wengine wa maendeleo wamekuwa msaada mkubwa katika kusaidia Ajenda ya Nishati Safi ya kupikia kuzidi  kusonga mbele hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati  akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko katika warsha ya nishati safi ya kupikia iliyoanza tarehe 19 Juni 2024 jijini Dar es Salaam.

“Serikali inatambua michango ya programu mbalimbali zinazotekelezwa na washirika wa maendeleo na sekta binafsi ikiwemo ya mradi wa CookFund unaoendelea katika nchi yetu. Katika kuendeleza sekta hii, tuko tayari kuendelea kushirikiana na UNCDF na wadau wengine wa nishati safi ya kupikia,” amesema Kapinga.

Aidha, amewataka wadau kushirikiana na serikali ili kwa pamoja kutafuta na kupendekeza mikakati ambayo itaharakisha lengo la nchi la asilimia 80 ya watanzania kutumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo 2034.

Amesisitiza kuwa, kila mmoja ana jukumu muhimu katika kufanikisha maendeleo ya soko na teknolojia zinazohitajika kufikia lengo hilo  la asilimia 80 ya Watanzania kuhamia kwenye Nishati Safi ifikapo 2034 kama ilivyoainishwa kwenye Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

“Warsha hii ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi 2024 – 2034, ambapo aliagiza Wizara ya Nishati kukaa pamoja na wadau wa Nishati Safi ya Kupikia na kuzungumzia kuhusu itakavyoweza kufikia kwa pamoja malengo ya mkakati wa nishati safi ya kupikia,” amesisitiza Kapinga.

Vile vile, amewataka wadau katika kuelekea katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kuwa wabunifu, waoneshe juhudi na kudumusha ushirikiano miongoni mwa wadau wa sekta ili kufikia lengo.

Ameongeza kuwa, Serikali itaweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia kwa kila kaya ili kuimarisha afya ya umma na maendeleo endelevu katika Sekta ya mazingira na uchumi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la UNCDF nchini, Peter Malika amesema wanashirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali ikiwemo mfuko wa CookFund unaolenga kuimarisha Nishati Safi ya Kupikia. Amesema Nishati Safi ni fursa na biashara ambapo  aliwataka wadau mbalimbali kuichangamkia fursa hiyo kwa sasa.

Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali, wakiwemo Watunga Sera, Wadau wa Maendeleo, Wabunifu, Sekta Binafsi na Washirika wa Kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari za SiasaKimataifa

30 wafariki dunia maandamano Kenya

Spread the loveShirika la Human Rights Watch limesema takriban watu 30 walifariki...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

error: Content is protected !!