Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 60 kujenga barabara ya Isongole – Kasumulu
Habari Mchanganyiko

Bilioni 60 kujenga barabara ya Isongole – Kasumulu

Spread the love

SERIKARI imetenga zaidi ya Sh 50 bilioni kujenga barabara kutoka Isongole wilayani Ileje mkoani Songwe hadi Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya yenye urefu wa kilometa 92 kwa kiwango cha lami. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe… (endelea).

Akizungumza leo tarehe 23 Oktoba 2023 Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema serikali imedhamiria kuifungua nchi kwa kujenga barabara maeneo mbalimbali ikiwemo ya Isongole hadi Kasumulu iliyopo kwenye mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Amesema mradi huo upo kwenye hatua za mwisho kuanza hasa ikizingatiwa ni mradi wa kimkakati kwani itakapokamilika utaongeza fursa za kiuchumi kwani mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira na magari yatapita kwenye njia hiyo kusafirisha bidhaa.

“Bidhaa nyingi zitakazotoka mkoa wa Ruvuma kupitia bandari ya Kyela- ziwa nyasa zitapita kwenye njia hiyo kwenda mikoa ya Rukwa, Katavi hadi Kigoma ikiwemo nchi ya Zambia badala ya kuzunguka njia ya Tanzam, pia itaimarisha ulinzi na nchi ya Malawi “amesema Kasekenya.

Ameongeza kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ni wakulima hivyo baada ya kuwezeshwa mbolea ya Ruzuku watanufaika zaidi kupita kwenye barabara nzuri kwenda kuuza mazao yao kwenye masoko yaliyopo mikoa mingine.

Meneja wa wakala wa barabara nchini (TANRODS ) mkoani Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga amesema ujenzi huo utaanzia na kilometa 52 na kwamba watahakikisha wanasimamia vyema mradi huo mkubwa ujengwe kwa viwango bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!