Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Mgeni ataka usimamizi  wa miradi ya maendeleo
Habari Mchanganyiko

DC Mgeni ataka usimamizi  wa miradi ya maendeleo

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka watendaji Serikali kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji, ili iweze kukamilika kwa wakati. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Alisema pamoja na fedha za mradi kupelekwa mradi huo haujaanza kufanya kazi  hali ambayo imelete malalamiko  kwa wananchi.

Mgeni aliwataka watendaji wote wanaohusika kuhakikisha mradi huo unakamilika ili kuondoa tatizo la maji kwa wananchi.

DC Mgeni alimtaka Meneja RUWASA Wilaya ya Same kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati, ili wananchi wapate huduma za maji.

Pia  amewataka  kunapotokea mabadiliko yoyote  katika sekta ya maji  ikiwemo kupanda kwa bili za maji  kutoka Sh. 2000 hadi 5000  kwa mwezi ambayo pia wananchi hawakuwa na uelewa kuhusiana na ongezeko hilo.

“Ni vema kutumia vikao vya kisheria   vya bodi ya maji kutoa ufafanuzi kwa wananchi badala ya kunyamaza na kuzua masuala mengi toka kwa wananchi,”alisema.

Wananchi walimweleza DC kuwa Waziri wa Maji Juma Awezo, aliagiza hapo Julai 2021 ukarabati ufanyike ndani ya miezi mitatu uwe umekamilika  ili wananchi waweze kupata huduma ya maji, lakini  mpaka sasa hawajui kinachoendelea kwani tatizo la maji liko  palepale  na  kwamba hawajui mradi huo umekamilika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!