Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwalimu matatani tuhuma za ubakaji mwanafunzi
Habari Mchanganyiko

Mwalimu matatani tuhuma za ubakaji mwanafunzi

Spread the love

 

MWALIMU Tunu Broun (37) wa shule ya msingi Senjele wilayani Mbozi mkoani Songwe amedaiwa kutokomea kusikojulikana akikwepa mkono wa sheria baada ya  kutuhumiwa kumfanyia ukatili kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa mika 14 (jina limehifadhiwa). Anaripoti Ibrahim Yassin, Songea (endelea).

Akizungumza leo tarehe 28 Aprili 2023 huku akitokwa na machozi, Babu anayeishi na mtoto huyo Julias Mwambipile amesema tarehe 17 Aprili 2023 asubuhi aliitwa shuleni na Mwalimu Broun ambapo alitii wito na kufika shuleni na kuelezwa kuwa mjukuu wake ni mtoro darasani.

Amesema baada ya kuelezwa tuhuma za mjukuu wake kuwa ni mtoro aliomba msamaha ambapo mwanafunzi huyo alisamehewa na kuruhusiwa kuingia darasani na yeye kurejea nyumbani.

Amesema mwanafunzi alikiri kuwa ni mtoro huku akidai alikuwa anaogopa kuchekwa na wenzake waliokuwa wakimuita jina la mama wa darasa jambo ambalo mwalimu wao aliwaonya.

Babu huyo mesema muda mfupi baada ga kurejea nyumbani alipata taarifa kuwa mjukuu wake amebakwa ndipo walipoenda kwa mwenyekiti wa kijiji.

Amefafanua kuwa tukio hilo la ubakaji lilijiri baada ya mwalimu huyo kumuamuru mwanafunzi huyo kwenda nyumbani kwake ambapo alipofika alianza kumuingilia kinguvu kwa madai ya kumsaidia darasani na kumpa uongozi wa shule, dada mkuu.

“Baada ya kufanyiwa ukatili huo, Mwalimu huyo alimuagiza mtoto huyo kurejea nyumbani lakini kutokana na maumivu makali yaliyomfanya kushindwa kutembea vizuri, msamaria mwema aliyekutana naye njiani alimhoji kisha kumueleza kilichomtokea.

“Msamaria mwema huyo aliamua kumpeleka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Senjele, Juma Shipela ambapo walifanyia mahojiano,”amesema.

Amesema waliamua kwenda shuleni hapo na kukuta mwalimu huyo mtuhumiwa ametokomea kusikojulikana.

Bibi wa muhanga Rose Mwampashi amesema wajukuu zake anawalea kwa taabu na alitegemea mwalimu angekuwa ni msaada kwa watoto ili wafikie ndoto zao za kielimu lakini sasa imekuwa kinyume.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Songwe, Theopista Malya amekiri kuwepo kwa tuhuma hizo za mwalimu kumbaka mwanafunzi wake.

Amesema tayari wamemfungulia jalada la uchunguzi huku wakiendelea kumsaka mwalimu huyo.

Amesema mwalimu huyo alitenda kosa hilo tarehe 17 April mwaka huu nyumbani kwake muda wa mchana huku akitumia mbinu ya kumlaghai kumsaidia kimasomo kutokana na maisha duni aliyonayo.

Malya amesema baada ya mtuhumiwa kutenda kosa hilo, ametoroka na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MWO/315/2023 na pindi atakapokamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Natoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto kwani vitendo hivyo vinafifisha ndoto zao.
Aidha, Kamanda Malya amewataka wananchi na jamii yote kwa ujumla kuacha vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto ambavyo vimezidi kukithiri mkoani Songwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!