Sunday , 30 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Biteko aipongeza TMA kwa kutoa huduma ya utabiri kwa ubora
Habari Mchanganyiko

Dk. Biteko aipongeza TMA kwa kutoa huduma ya utabiri kwa ubora

Spread the love

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameipongeza Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuendelea kutoa huduma bora za hali ya hewa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema hayo wakati alipotembelea banda la TMA kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani,yanayo fanyika katika viwanja vya JICC, mjini Dodoma.

Dk.Biteko alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maadhimisho haya muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya mazingira nchini na alitembelea Banda la TMA na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dk. Ladislaus Chang’a.

“Hongereni sana kwa huduma bora za utabiri mnazitoa kila siku na zinatusaidia sana, hongereni sana,” alisema Dk. Biteko

Kwa upande wake Dk. Chang’a aliwaomba wananchi wa Dodoma na wale wa mikoa ya jirani watumie fursaha hii kwa kutembelea banda la TMA kwenye maadhimisho haya ili kujifunza maswala mbalimbali ya mazingira na masuala mbalimbali ya hali ya hewa , na huduma zitolewazo na TMA.

“Karibuni wananchi wote katika banda la TMA, mje kujifunza na kuongeza uelewa wa huduma za hali ya hewa na matumizi yake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii. Kujifunza uhusiano wa hali ya hewa na mazingira yanayotuzunguka. Tunao wataalam bingwa wa hali ya hewa na wapo tayari kutoa elimu,” alisema Dk. Chang’a

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya wiki ya Mazingira kwa mwaka 2024 yenye kauli Mbiu “urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Mpina amng’ang’ania Bashe, kumburuza mahakamani pamoja na bodi ya sukari

Spread the loveMbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema amenuia kumpeleka mahakamani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Majahazi yadakwa na madumu 1,731 ya mafuta ya kupikia

Spread the loveKikosi kazi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam kimekamata majahazi...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye ualbino wafikishwa mahakamani

Spread the loveWATUHUMIWA wa mauaji ya Asimwe Novath, mtoto mwenye ualbino, wamefikishwa...

Habari Mchanganyiko

Sangoma awaponza vijeba, watupwa jela maisha kwa kubaka wanafunzi

Spread the loveMAHAKAMA ya wilaya Nkasi Mkoani Rukwa, imemhukumu kifungo cha maisha...

error: Content is protected !!