PROF. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum (Ikulu), ameteuliwa kuwa mrithi wa William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu. Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).
Lukuvi (70), alifariki dunia, Jumatano ya wiki iliyopita, katika hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma na amezikwa kijijini kwake, Idodi, mkoani Iringa. Alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na shinikizo la moyo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, imeeleza kuwa mbali na Prof. Kabudi, rais Samia amefanya uteuzi, uhamisho na utenguzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia amemhamisha Reuben Kwangilwa, kutoka ofisi ya waziri mkuu, kwenda ofisi ya makamu wa rais.
Kwangilwa alikuwa naibu Waziri katika wizara hiyo na anaendelea na wadhifa wake huko katika wizara yake mpya.
Naye Dk. Festo Dugange, aliyekuwa naibu Waziri mkuu, ofisi ya makamu wa rais, amehamishiwa ofisi ya waziri mkuu.
Balozi Ali Jabir Mwadini, amefanywa kuwa Katibu wa Rais (KR); Dk. Eveline Munisi na Angela Kiziga, wameteuliwa kuwa wabunge katika Bunge la Muungano; Balozi Said Yakub, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Comoro, amefanywa kuwa balozi nchini Ufaransa.
Dk. Evaline Munisi, alikuwa mgombea Mwenza wa urais, “katika uchaguzi uliofanyika 29 Oktoba mwaka jana,” kupitia NCCR – Mageuzi.
Katika taarifa hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi anasema, James Mwainyekule, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ameondolewa ofisini.
Taarifa ta Ikulu imesema, Mwainyekule atapangiwa majumu mengine.
Hata hivyo, hakuna maelezo ya sababu za kuondoshwa kazini mkurugenzi mkuu wa EWUFRA, ingawa utenguzi wake umefanyika huku mamlaka hiyo, ikipandisha bei ya mafuta.
Serikali nchini Tanzania ilitangaza bei mpya ya juu ya mafuta iliyoanza kutumika jana Jumatano, tarehe 1 Aprili 2026, ambapo bidhaa hiyo ilipanda kwa zaidi ya Sh. 956 kwa kila lita ya dizeli na petroli na kuzua hisia kali miongoni mwa raia.
Kulingana na EWURA, kupanda kwa bei hizo kumetokana na ongezeko kubwa linalosababishwa na mzozo unaoendelea Mashariki ya kati dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa bei mpya mjini Dar es Salaam Petroli sasa itauzwa kwa shilingi za Tanzania 3,820, Dizeli Sh 3,806, Mafuta ya Taa Sh 3,684.
ZINAZOFANANA
Mahakama Bunda yamuachia Katibu Bavicha, wenzake 13
Watu 518 waliuawa 29 Oktoba
Ripoti ya Tume yasubiriwa