KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo amewataka viongozi wa Equatorial Guinea kutoitumia haki kama chombo cha kutopkea adhabu pekee, akisisitiza kuwa mfumo wa haki unapaswa kulinda jamii, na kwamba hakuna haki bila maridhiano.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Papa Leo ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika gereza maarufu katikamji mkuu wa uchumi, Bata. Amesema “Haki ya kweli haitafuti kuadhibu bali kusaidia kujenga upya maisha ya waathiriwa, wahalifu na jamii zilizojeruhiwa na uovu,” Papa Leo amesisitiza. Maoni hayo yalifuatia ukosoaji wake wa awali wa hali ya wafungwa katika magereza ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ambayo makundi ya haki za binadamu yanasema iko chini ya utawala wa kimabavu. Akizungumza na mamia ya wafungwa waliokusanyika kwenye uwanja wa gereza, papa amewahimiza wasikate tamaa, akisema, “hamko peke yenu.” “Familia zenu zinawapenda na zinawasubiri. Watu wengi nje ya kuta hizi wanawaombea,” amesema. Makundi ya haki za binadamu yanasema gereza hilo linatumika kuwanyima wapinzani na wakosoaji wa kisiasa uhuru wao, huku Amnesty International ikifichua kwamba wafungwa wanaripotiwa kupigwa mara kwa mara. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Marekani itaendelea kuweka kizuizi cha kijeshi Hormuz-Trump