RIPOTI mpya ya Freedom House ya 2025 yaziorodhesha kwa mara ya kwanza Tanzania na Kenya miongoni mwa nchi zinazotuhumiwa kuwakandamiza raia wao nje ya mipaka.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Ripoti hiyo yaeleza kuwa serikali zinadaiwa kuwafuatilia, kuwakamata au kuwarejesha kwa nguvu wakosoaji waliokimbilia ughaibuni vitendo vinavyojulikana kama ukandamizaji wa kuvuka mipaka. Afrika Mashariki imeibuka kama moja ya vitovu vya vitendo hivyo, huku takribani nchi 54 duniani zaidi ya robo ya mataifa yote zikihusishwa na matukio hayo tangu mwaka 2014. Kwa mujibu wa utafiti huo, China inaongoza duniani, ikifuatiwa na Vietnam na Urusi, wakati Kenya na Tanzania zikiorodheshwa kwa mara ya kwanza pamoja na mataifa mengine kama Afghanistan na Zimbabwe. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Malema ahukumiwa miaka mitano gerezani Mpina akutana na Chakwera,aibua tuhuma dhidi ya uchaguzi