MAHAKAMA nchini Afrika Kusini leo imemhukumu kiongozi wa upinzani Julius Malema, kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kufyatua risasi kwa kutumia bunduki ya kivita katika mkutano wa hadhara miaka minane iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Mamia ya wafuasi waliovaa mavazi mekundu ya chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) walijikusanya nje ya mahakama wakati hukumu hiyo ikitolewa, katika kesi iliyokuwa na mvutano mkubwa wa kisiasa. Hakimu Twanet Olivier alisema Malema alivunja sheria za umiliki na matumizi ya silaha kwa makusudi, baada ya kufyatua risasi angani mwaka 2018 wakati wa maadhimisho ya chama chake cha EFF. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation China yailaumu Marekani kudhibiti bandari za Iran Tanzania na kenya zatajwa ukandamizaji dhidi ya raia nje ya nchi-ripoti