MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameibuka na agizo jipya lenye uzito wa kisiasa, akiwataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kuanza mara moja maandalizi ya mikutano ya hadhara nchi nzima.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Lissu ametoa kauli hiyo leo akiwa katika Gereza la Ukonga baada ya kufanya mazungumzo na wakili wake, Paul Kisabo, kuhusu mwenendo wa kesi zinazomkabili pamoja na hatima ya shughuli za chama hicho. Katika hatua hiyo, Lissu amepokea na kupitia uamuzi wa Mahakama ya Rufani Tanzania uliotolewa 15 Aprili 2026, ambao umeondoa vikwazo kwa Chadema na kuruhusu chama hicho kuendelea na shughuli zake za kisiasa. Akizungumzia uamuzi huo, Lissu amesema ni muda wa kurejea kwa nguvu kwenye majukwaa ya siasa, akisisitiza kuwa mapambano ya kudai haki, demokrasia na utawala bora hayawezi kusubiri tena. Katika maelezo yake, kiongozi huyo pia amefichua hoja saba alizowasilisha kwa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, akieleza kuwa kesi ya uhaini inayomkabili inahusiana moja kwa moja na msimamo wake wa “No Reforms, No Election”. Miongoni mwa mambo aliyosisitiza ni kufutwa kwa kesi zote dhidi yake na chama, kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya Oktoba 2025 kupitia taasisi kama SADC, pamoja na mageuzi ya kina ya mfumo wa uchaguzi na vyombo vya ulinzi na usalama. Lissu amehitimisha kwa kutoa wito wa kupatikana kwa Katiba Mpya na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, akieleza kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya kweli yatakayofanyika katika mazingira ya uhuru na haki. Kwa upande wake, Chadema kimesisitiza kuwa kitaendelea kupigania mageuzi ya kisiasa kwa njia za amani na kisheria, huku maandalizi ya mikutano ya hadhara yakitarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa kote nchini. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Mpina akutana na Chakwera,aibua tuhuma dhidi ya uchaguzi Lissu aja na masharti ya mazungumzo, ataja Katiba mpya, kufutwa kwa tume ya Uchaguzi