TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemuambia mjumbe wa Jumuiya ya madola, Dk. Lazarus Chakwera kuwa ili Tanzania kupatikane maridhiano ya dhati inahitaji mabadiliko katika mifumo ya kiuchaguzi, katika vyombo vya ulinzi na usalama na Katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Mkurugenzi wa mawasiliano ya umma wa Chadema, Brenda Rupia, amesema kuwa mazungumzo ya Lissu na Chakwera yalifanyika jana tarehe 15 Aprili 2026, katika Gereza Kuu la Ukonga, jijini Dar es Salaam anaposhikiliwa kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani. Katika taarifa ya Rupia amesema kuwa Lissu amemueleza Dk. Chakwera, kuwa yupo tayari kwa mazungumzo akiwa mtu huru na kwamba kesi inayomkabili kwa mwaka mmoja sasa inatokana na msimamo wake na chama chake wa kupinga uchaguzi mpaka pale kutakapokuwa na mabadiliko ya kimfumo yaani No Reforms No Election. Lissu amesisitiza mazungumzo yanayokubalika ni yale yatakayokuwepo katika mazingira wezeshi yenye ukweli na yenye kutekelezeka. Aidha Lissu amemwambia Dk. Chakwera kuwa matukio yote ya Oktoba 2025 yafanyiwe uchunguzi huru kupitia chombo cha kimataifa, kama vile SADC. Pamoja na uwajibikaji wa kitaasisi kwa yaliyotokea Oktoba 2025, mfano, Ofisi ya Msajili, INEC na TCRA, alisisitiza umuhimu wa kurejea Ripoti ya Jaji Nyalali (1992). Lissu amemwambia Dk. Chakwera kuwa kuwepo kwa mabadilika ya lazima kwenye vyombo vya dola huku akitaja ripoti ya Jaji Chande ya haki jinai iwe dira kwenye eneo hilo sambamba na mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi huku akisisitiza kurejea ripoti za waangalizi wa uchaguzi (1995–2025), pamoja na Ripoti za Jaji Warioba na Jaji Nyalali. Lissu alimwambia Dk. Chakwera kuwa matatizo yote yanatokana na Katiba hivyo amesisitiza kupatikana kwa Katiba Mpya itakayotokana na matakwa ya wananchi na sio watawala. Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema, Wakili Gaston Galubindi amefafanua kwa kirefu mazungumzo ya Lissu na Dk. Chakwera tunakualika kusikiliza Kupitia Youtube channel ya MwanaHALISI TV Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Chadema kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima