Mwenyekiti wa Tume, Jaji mkuu mstaafu Mohamed Chande

 

HATIMAYE macho na masikio ya Watanzania yanaelekezwa kwenye ripoti ya Tume ya Rais ya Uchunguzi wa mauaji ya 29 Oktoba mwaka jana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tume hiyo, inatarajiwa kukabidhi ripoti yake ya uchunguzi inatarajiwa kukabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Jaji mkuu mstaafu Mohamed Chande, ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi wa kina uliogusa pande mbalimbali za jamii.

Kauli za awali kutoka kwa rais zilieleza madai kuwa baadhi ya vijana waliingia mitaani kwa kushawishiwa kifedha, huku wengine wakidaiwa kufuata mkumbo bila kuelewa undani wa walichokuwa wakikifanya.

Ripoti hii inachukuliwa kama nyenzo muhimu ya kuweka wazi ukweli na kutoa mwelekeo wa taifa baada ya kipindi hicho kigumu.

Kwa wengi, ni fursa ya kupata majibu sahihi na kujenga imani upya kwa taasisi za nchi, huku ikibeba matumaini ya kuimarisha uwazi, haki na mshikamano wa kitaifa.

Tayari viongozi mbalimbali wameanza kuripoti Ikulu, kushiriki hafla hiyo, huku kukiwa kumeanza kampeni kabambe yenye lengo la kutetea ripoti ambayo bado ilikuwa haijatoka hadharani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!