Hilda Newton

 

JESHI la Polisi nchini Tanzania, limesema linaendelea na uchunguzi wa kukusanya ushahidi kutokana na taarifa ya Hilda Newton, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anayedai kuwapo njama za kutaka kuangamiza maisha ya Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Newton anadaiwa na jeshi hilo, kuchapisha na kusambaza taarifa katika m mitandao ya kijamii, inayodai kuwapo mkakati wa kumdhulu Mwenyekiti huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini.

Newton alichapisha taarifa hiyo, tarehe 10 Aprili mwaka huu, kupitia mitandao kadhaa ya kijamii.

Katika taarifa yake hiyo, Newton alisema: “Serikali imepanga kumuua Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kwa risasi hivyo Ili kukamilisha uchunguzi.”

Jeshi la Polisi limemuwelekeza Newton kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai iliyopo katika jengo la Makao Makuu Ndogo ya Polisi iliyopo Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam, tarehe 24 Aprili 2026 saa 4 asubuhi ili aweze kuwasilisha ushahidi aliosema na kutangazia umma.

Jeshi la polisi limesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 11 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!