RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema nchi yake itaendelea kutekeleza kizuizi cha kijeshi dhidi ya Iran, licha ya kufunguliwa mlango wa Hormuz kwa shughuli za kibiashara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).

Kupitia ujumbe aliouchapisha jana Ijumaa 17 Aprili 2026 katika mtandao wa Truth Social, Trump alisisitiza kuwa hatua za kijeshi hazitasitishwa hadi pale makubaliano kamili yatakapofikiwa kati ya pande hizo mbili.

“Lakini kizuizi cha kijeshi kitaendelea kutekelezwa kwa nguvu zote, hadi pale tutakapoafikiana na Iran kwa asilimia 100,” ameandika Trump, akionyesha msimamo mkali wa Washington katika mazungumzo yanayoendelea.

Hata hivyo, Trump alieleza kuwa kuna matumaini ya kufikia makubaliano, akidai kuwa sehemu kubwa ya masuala yenye utata tayari yamejadiliwa na kufikiwa mwafaka.

Serikali ya Iran jana ilitangaza kufungua mlango wa Hormuz kwa shughuli za usafirishaji wa kibiashara, wakati mazungumzo na Marekani yakiendelea kuhusu usitishaji mapigano.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!