Dk. Festo Dugange
RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteuwa Reuben Kwagilwa, kuwa Naibu Waziri wa Nchi, katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kabla ya mabadiliko hayo, Kwagilwa, alikuwa Naibu Waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Taarifa ya uhamisho huo, imetolewa leo tarehe 2 Aprili 2026 na Balozi Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi.
Katika mabadiliko hayo, Dk. Festo Dugange, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), amepelekwa Tamisemi kuendelea na wadhifa wake wa naibu waziri.
ZINAZOFANANA
Mahakama Bunda yamuachia Katibu Bavicha, wenzake 13
Watu 518 waliuawa 29 Oktoba
Ripoti ya Tume yasubiriwa