Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kondomu kupanda bei

BEI ya kondomu huenda ikapanda kutokana na vita vinavyoendelea eneo la Mashariki ya Kati ambako Marekani na Israel, vinashambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kupanda bei kwa bidhaa hiyo, kunatokana na viwanda vingi vikiwamo vya kodomu, kukumbana na na athari za vita hivyo.

Usumbufu katika usambazaji wa amonia na mafuta ya silikoni, bidhaa zinazotoka na petroli zinazotumika katika utengenezaji wa kondomu, umesababisha hatari ya kupanda kwa bei, wanaeleza wachambuzi wa uchumi na “hilo inaweza pia kuathiri mauzo ya rejareja.”

Kuna dalili za kutosha kutoka kwa wauzaji nchini India, kwamba bei ya amonia inaweza kuongezeka kwa asilimia 40-50, kutokana na hilo bei ya mafuta ya silikoni inaweza pia kuongezeka.

Afisa mmoja anayehusika na biashara hiyo ameiambia BBC kwa sharti la kutotajwa jina, kwamba “hakuna mtu aliyefikiria kungekuwa na tatizo lolote katika kondomu.”

Amonia hutumika kuimarisha mpira na kuondoa protini iliyozidi. Mafuta ya silikoni hufanya kazi kama mafuta ya kulainisha kondomu.

About The Author

error: Content is protected !!