
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetaja mambo kumi ya msingi ambayo yamesababisha kituo hicho kupaa kiuchumi barani Afrika ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Gilread Teri akitoa taarifa ya utekelezaji wa mafanikio ya kituo hicho kwa miaka minne amesema kuwa njia pekee iliyofanikisha mafanikio makubwa ni pamoja na kutoa kipaumbele kwa sekta binafsi hususami wazawa.
Jambo lingine ambalo ameeleza kuwa limechangia maendeleo na mafanikio katika kituo hicho ni pamoja na ubadolishaji wa sheria ya uwekezaji ambayo ni sheria ya uwekezaji na maboresho ya maboresho ya ubia binafsi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Teri amesema kuwa Mtanzania mwenye kukithi vigezo vya uwekezaji na mwenye mtaji wa shilingi milioni 100 anatambuliwa na kupewa sifa ya uwekezaji.
Amesema kuwa mtanzania mwenye taarifa ya benki yenye kiasi cha fedha kiasi cha milioni kumi benki kwa miezi mitatu hadi sita kwa kuonesha mzunguko wa kutoka na kuingia unapewa sifa na kuwa na kigezo cha kuwekeza.
Amesema mafanikio mengine ya TIC ni pamoja maboresho ya kuwahudumia watanzania kwa kuongeza ueledi pamoja na kuongeza makusanyo ya kila mwezi kutola shilingi milioni 400 kwa mwezi mwaka 2022 na kufikia shilingi bilioni 1 kwa mwezi kwa mwaka 2024 na kufanikiwa kukusanya shilingo bilioni 12 kwa mwaka 2024.
Akizungumzia fanikio la nne Teri amesema ni kukuza diplomasia ya uchumi na kufanyika ziahara za kimkakati zinazoshawishi uwekezaji wa watu kutoka katika mataifa mbalimbali na balozi zote 44 kufanya changamfu kwa kuwavutia wawekezaji nchini.
Aidha amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la mtaji,viwanda na ajira pamoja na kuongezeka kwa teknologia sambamba na uwekezaji kwenda Mikoa yote ya Tanzania pia kumekuwepo na ongezeko la wawekezaji mahiri na muhimu,kuongezeka kwa wawekezaji wa ndani na kuwepo kwa uwekezaji mtambuka nchini tofauti na nchi nyingine Duniani.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yashirikiana na jamii kupanda miti
Mwana FA aivulia kofia Serikali ya Rais Samia
Lissu mgeni rasmi Siku ya Wanawake Duniani Mlimani City