October 16, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais wa Comoro achomwa kisu

Azali Assoumani

 

RAIS wa Comoro, Azali Assoumani amejeruhiwa katika shambulio la kisu, mamlaka zimesema.
“Asante Mungu, maisha yake hayako hatarini,” amesema msemaji wa serikali. MORONI, Comoro

Alidungwa kisu alipokuwa akihudhuria mazishi ya kiongozi wa kidini karibu na mji mkuu Moroni lakini “alijeruhiwa kidogo” na amerejea nyumbani, msemaji Fatima Ahamada aliambia shirika la habari la Reuters.

Aliongeza kuwa mshambuliaji alikamatwa.

About The Author