Hashim Kambi, afariki dunia
MUIGIZAJI maarufu na mkongwe nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia. Alikuwa amezidiwa l ghafla wakati akifanya shughuli zake za kurekodi studio.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Hashim Kambi alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliolitumikia kwa muda mrefu tasnia ya Bongo Movie, akijizolea heshima kubwa kutokana na umahiri wake wa uigizaji hasa kwenye eneo la mafundisho ya kijamii.
Kupitia kazi zake, ameacha alama ya kudumu kwenye mioyo ya watazamaji wengi, huku akichukuliwa kama mmoja wa waasisi na walezi wa vipaji vipya ndani ya tasnia ya filamu nchini.
Taarifa zinasema, Kambi amefikwa na mauti akiwa hospitalinu na kwamba na taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia na wadau wa filamu baada ya kukamilika kwa mashauriano.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.