Rais Trump, Vance chupuchupu kuuawa
Rais wa Marekani, Donald Trump na Makamu wake JD Vance
Rais wa Marekani Donald Trump, Makamu wake JD Vance na maofisa wengine wa serikali walikimbizwa katika eneo salama baada ya milio ya risasi kusikika kwenye ukumbi ambapo walikuwa wakihudhuria halfa moja jijini Washington usiku wa kuamkia leo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kulingana na video zilizonaswa kutoka kwenye eneo ambalo tukio hilo limetokea, maofisa wa usalama wanaonekana wakimuondoa kwa dharura Trump pamoja na JD Vance baada ya milio ya risasi kusikika. Wengine waliokuwemo pia walihamishiwa kwenye eneo salama.
Mtu aliyekuwa amejihami kwa silaha, alijaribu kupita kizuizi cha walinda usalama nje ya ukumbi ambapo halfa hiyo ilikuwa ikifanyika kabla maofisa wa usalama wa Marekani kumzidia nguvu.
Wageni wengine wanaonekana wakijificha chini ya meza wakati vurugu zilipoaanza.
Baada ya tukio hilo Rais Trump amethibitisha kuwa mshukiwa aliyekuwa amejihami kwa bastola amekamatwa, akichapisha picha zake kwenye mitandao yake ya kijamii.