Rais Traore alaani mashambulizi ya kigaidi nchini Mali
Kapteni Ibrahim Traore, kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso
RAIS wa Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES), Ibrahim Traoré, ambaye pia ni Rais wa Burkina Faso, amelaani mashambulizi ya “kigaidi” yaliyofanyika nchini Mali 25 Aprili 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mashambulizi hayo yanaripotiwa kufanywa na wapiganaji wanaohusishwa na kundi la JNIM, pamoja na wapiganaji wanaotaka kujitenga wa Tuareg.
Katika taarifa hiyo iliyosainiwa 25 Aprili 2026,Traoré alisema mashambulizi hayo yalilenga maeneo mbalimbali ndani ya ardhi ya Mali na yalikuwa sehemu ya mkakati mpana wa uchokozi dhidi ya kanda ya Sahel katika juhudi zake za kujipatia uhuru wa kujitawala