Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Askari aliyemkamata Rais wa Venezuela akamatwa

 

ASKARI wa kikosi maalum cha Jeshi la Marekani, Gannon Ken Van Dyke, amekamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kutumia taarifa za siri za kijeshi kujipatia fedha kupitia kamari ya mtandaoni iliyohusiana na operesheni ya kumkamata aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka nchini Marekani, Van Dyke alitumia taarifa alizozipata kazini kuhusu operesheni hiyo kabla haijatangazwa rasmi kwa umma, na kisha akaweka dau katika jukwaa la kamari ya utabiri wa matukio ya kisiasa (prediction market). Inadaiwa kuwa alifanikiwa kushinda zaidi ya dola 400,000 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja.

Uchunguzi unaeleza kuwa askari huyo alikiuka sheria kwa kutumia taarifa nyeti za serikali kwa manufaa binafsi, jambo ambalo linachukuliwa kama kosa kubwa la jinai hasa kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Van Dyke sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya taarifa za siri, udanganyifu wa kielektroniki (wire fraud), pamoja na udanganyifu wa kifedha.
Endapo atapatikana na hatia, anaweza kukabiliwa na adhabu kali ikiwemo kifungo cha muda mrefu gerezani.

About The Author

error: Content is protected !!