MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda imetoa uamuzi mdogo katika kesi ya jinai inayomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa BAVICHA Taifa, Yohana Kaunya na wenzake 20, ambapo washtakiwa 14 wameachiwa huru baada ya kubainika hawana hatia.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mulokozi Kamuntu, aliyesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha kuwahusisha washtakiwa hao na makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, maandamano na uchomaji moto.

Hata hivyo, Kaunya na washtakiwa wengine sita wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka ya kujeruhi, uharibifu wa mali na baadhi ya makosa ya uchomaji moto, baada ya mahakama kuridhika kuwa kuna ushahidi wa awali unaowalazimu kujitetea.

Mahakama pia imewatia hatiani bila kesi ya kujibu washtakiwa wote katika kosa la wizi wa kutumia silaha, hivyo kuwaachia huru kwa shtaka hilo ambalo halina dhamana, na kubaki na makosa yanayoruhusu dhamana kisheria.

Kutokana na hali hiyo, mahakama imewapa dhamana washtakiwa saba waliobaki kwa masharti maalum yaliyowekwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi 23 Aprili 2026, ambapo hatua ya utetezi inatarajiwa kuanza rasmi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!