MWANAMKE Monica Beda (36), mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha shilingi milioni 60.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea). Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo 20 Aprili 2026 na Wakili wa Serikali Cathbert Mbiling’i imeileza mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo 8 Novemba 2025, katika Mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Salome Mshasha, imedaiwa mshtakiwa alimlaghai Agrey Festo Mashanda kwa kujifanya angeweza kumuagizia gari aina ya Mitsubishi Fuso Fighter Damper lenye chassis namba FK418F-550031, huku akijua kuwa si kweli. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo umekamilika na wameomba kupangiwa tarehe kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (PH). Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana Mahakama ilimpatia mshtakiwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, ambapo mmoja wao anatakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika au fedha taslimu yenye thamani ya nusu ya fedha anazodaiwa kuiba, sawa na shilingi milioni 30. Kesi hiyo limeahirishwa hadi 6 Mei 2026 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Ripoti ya LHRC: Machafuko ya Oktaba 29 yametia doa Chadema yamshtaki Samia kwa wanwake viongozi wa Afrika