KITUO cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC), kimesema machafuko yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa 29 Oktaba 2026 na baada ya uchaguzi huo, yamelitia doa taifa kwenye uga wa haki za binadamu. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa kwenye ripoti ya haki za binadamu ya shirika hilo kwa mwaka 2025. Ripoti imeangazia yaliyotokea wakati wa uchaguzi huo na jinsi hali ya haki za binadamu ilivyodorora kwa kiwango kikubwa nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, leo tarehe 20 Aprili 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Anna Henga, amesema kuwa machafuko hayo, yamechafua tawira ya Tanzania mbele ya ulimwengu.

Alisema: “Yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, yametia doa Tanzania mbele ya uso wa ulimwengu. Hali hii imetokana na ongezeko la matendoa ya ukiukwaji wa haki za kiraia na kisiasa, ikiwemo haki ya kuishi, haki ya uhuru, usalama, usawa mbele ya sheria na uhuru wa kujieleza.”

Kwa mujibu wa Dk. Henga, katika kipindi hicho matukio ya utekaji, mauaji, kujeruhi na ukamataji kinyume cha sheria yaliripotiwa kwa wingi.

Ameongeza: “Matukio haya yaliibua hali ya wasiwasi kuhusu ulinzi wa haki za msingi za kibinadamu, ikiwemo haki ya kuishi na kukusanyika kwa amani.”

Ripoti hiyo imeonesha ongezeko la matukio ya utekaji, na upoteaji wa watu ambapo LHRC imesema kuwa imekusanya matukio 80 ya mwaka 2025 yakiwahusisha wanasiasa, wanahabari na wananchi wakawaida.

Dk. Henga ripoti hiyo haikusahau eneo la ukamataji holela na ucheleweshaji wa mashauri na vikwazo vya upatikaji msaada wa kisheria.

“Ripoti yetu haikukaa kimya, imetoa suluhisho kwa kutoa mapendekezo kwa mamlaka kwa kuchukua hatua za haraka, madhubuthi na za kimkati ili kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu,” amefafanua.

Amesema, “ripoti imetaka kufanyika kwa uchunguzi huru, na wa wazi na kwa muda maalum kuhusu matukio yote ya mauaji, utekaji, na upoteaji wa watu yaliyotukio kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.”

Shirika hilo linalojihusisha na utetezi wa haki za binadamu, limehimiza kuanza kwa mfumo wa kuiwajibikaji kwa vyombo vya dola ikiwemo kuanzishwa kwa chombo huru cha kiraia cha kusimamia utendaji wa maofisa wa vyombo vya usalama.

Aidha, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimmetaka kufanyika maboresho ya kisheria na kisera ili kulinda haki za binadamu na uhuru wa kijieleza.

“Mbali na haya ya ukiukwaji wa haki za binadamu, LHRC inataka kuongezwa jitihada za kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.”

Ripoti ya LHRC imetoka katika kipindi ambacho wananchi wanasubiri kwa hamu ripoti ya Tume ya Rais ya Uchunguzi wa kinachoitwa, “matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba mwaka jana.”

Tume ya Rais ya uchunguzi wa matukio ya 29 Oktoba mwaka jana, ‎inaongozwa na Jaji mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othuman.

https://youtu.be/xraWKNCjT-Y

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!