Climate

Mahakama yamkatalia Lissu kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali
Mahakama yamkatalia Lissu kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali

 

WAKILI Rugemeleza Nshala amesema Mahakama imetoa uamuzi mdogo kuhusu maombi ya Tundu Lissu ya kuomba kuunganishwa katika kesi namba 8323 iliyofunguliwa na Said Issa na wenzake, inayohusu mgawanyo wa mali.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Akiongea na waandishi wa habari hii leo tarehe 30 April 2026,Wakili Nshala amesema Mahakama imebaini kuwa Lissu aliwasilisha maombi hayo kwa nafsi yake binafsi na si kwa niaba ya nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama. Kutokana na hilo, Mahakama imehitimisha kuwa hana maslahi ya moja kwa moja katika shauri hilo, na hivyo kukataa ombi lake la kuunganishwa kwenye kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama imeeleza kuwa Lissu anaweza kushiriki katika shauri hilo kama shahidi endapo itahitajika.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa kesi hiyo sasa ipo mbele ya Jaji Ngunyale, badala ya Jaji Hamidu Mwanga kama ilivyokuwa awali.
Kesi hiyo itatajwa tena 13 Mei 2026 kwa ajili ya maagizo ya Mahakama, ikiwemo kujadili iwapo ilifunguliwa ndani ya muda wa kisheria wa miaka sita tangu mgogoro huo ulipoanza.

Rugemeleza Nshala, amesema Mahakama imetoa uamuzi mdogo kuhusu maombi ya Lissu ya kuomba kuunganishwa katika kesi namba 8323 iliyoletwa na Said Issa na wenzake hao, kuhusu mgawanyo wa mali.

Aidha, kesi hiyo sasa ipo mbele ya Jaji Ngunyale na si Jaji Hamidu Mwanga kama awali ma Itatajwa tena 13 Mei 2026 kwa ajili ya maagizo, ikiwemo kujadili iwapo iliwasilishwa ndani ya muda wa kisheria wa miaka sita tangu mgogoro ulipoanza.

Mwandishi wa habari jela miaka 60 kwa kukutwa na bangi
Mwandishi wa habari jela miaka 60 kwa kukutwa na bangi
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
Rais Ruto kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5
Rais Ruto kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5

News Analysis

Meridianbet yazidi kukimbiza kama chaguo la vijana wanaotaka burudani
Meridianbet yazidi kukimbiza kama chaguo la vijana wanaotaka burudani

Kwa kizazi cha sasa, kila kitu kinahitaji kuwa na maana, na Meridianbet imejidhihirisha kuwa zaidi ya sehemu ya kubeti. Ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya 2026, Meridian Holdings imeingiza zaidi ya dola milioni 50 kama faida. Hii inaonyesha wazi kuwa hapa ni jukwaa linaloleta matokeo na kuaminika kimataifa.

Nguvu kubwa ya mafanikio haya inatoka Meridianbet yenyewe, ambayo imeingiza dola milioni 34.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kutoka mwaka uliopita. Hii inaashiria kuwa vijana wengi wanaona thamani halisi hapa, wanajiunga, wanacheza, na wanapata ushindi. Ni sehemu ambayo burudani na fursa vinakutana.

Meridianbet wanakupa jukwaa pana la kubashiri, mechi kali za kimataifa hadi michezo ya kasino mtandaoni iliyojaa burudani. Ukiwa na odds zenye ushindani mkubwa, kila tiketi inakuwa na thamani zaidi. Jiunge sasa kupitia tovuti yao au piga *149*10#.

Ukuaji wa watumiaji wapya unaongeza uthibitisho huo. Karibu watu laki tano wamejiunga ndani ya muda mfupi tu, wakichagua Meridianbet kama jukwaa lao la kila siku. Hapa unakuwa sehemu ya jamii kubwa ya vijana wanaotafuta ushindi na kufurahia kila hatua ya mchezo.

Kwa zaidi ya miaka 25 ya uzoefu, Meridianbet imejenga jina kubwa duniani kuanzia Afrika, Ulaya na Amerika. Mfumo wake wa kisasa unakupa urahisi wa kubeti muda wowote, ukiwa popote, kwa usalama wa hali ya juu. Ni teknolojia iliyoundwa kumrahisishia mchezaji na kumpa uzoefu bora kila siku.

Huu ndio wakati wako wa kuchukua hatua na kuingia kwenye ulimwengu wa fursa. Jisajili Meridianbet leo, anza kubeti, na uwe sehemu ya vijana wanaoandika historia yao ya ushindi. Meridianbet si mchezo tu, ni nafasi ya kwenda mbele.

RC Singida apongeza jitihada za NBC kuchochea kasi ya mapinduzi ya kilimo
RC Singida apongeza jitihada za NBC kuchochea kasi ya mapinduzi ya kilimo
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
Meridianbet na uwekezaji wa utu kwa wagonjwa Mwananyamala
Meridianbet na uwekezaji wa utu kwa wagonjwa Mwananyamala

Latest News

error: Content is protected !!