MAHAKAMA ya wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, imemhukumu kifungo cha miaka 60 gerezani, Zawadi Jackson Mwakijolo, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha bangi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea). Mwakijolo, ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha 94.1 Keifo Fm, kilichopo mkoani Mbeya. Alikamatwa na askari polisi akiwa anasafirisha vifurushi 142 vya dawa za kulevya aina ya bangi vyenye uzito wa kilo 155.84, kutokea kivuko kisicho rasmi cha January kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali ya nchi kufanya biashara hiyo haramu. Akisoma uamuzi wa kesi hiyo, jana tarehe 29 Aprili 2026, Hakim Mkuu wa Mahakama ya wilaya ya Kyera, Paul Mabula Barnabas, ameeleza kuwa alitenda kosa hilo tarehe 2 Februari 2025. Kwa mujibu wa Mahakama, mshitakiwa ametiwa hatiani na amehukumiwa kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe Mahakama yamkatalia Lissu kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali