Climate

Mwandishi wa habari jela miaka 60 kwa kukutwa na bangi
Mwandishi wa habari jela miaka 60 kwa kukutwa na bangi

 

MAHAKAMA ya wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, imemhukumu kifungo cha miaka 60 gerezani, Zawadi Jackson Mwakijolo, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha bangi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Mwakijolo, ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha 94.1 Keifo Fm, kilichopo mkoani Mbeya.

Alikamatwa na askari polisi akiwa anasafirisha vifurushi 142 vya dawa za kulevya aina ya bangi vyenye uzito wa kilo 155.84, kutokea kivuko kisicho rasmi cha January kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali ya nchi kufanya biashara hiyo haramu.

Akisoma uamuzi wa kesi hiyo, jana tarehe 29 Aprili 2026, Hakim Mkuu wa Mahakama ya wilaya ya Kyera, Paul Mabula Barnabas, ameeleza kuwa  alitenda kosa hilo tarehe 2 Februari 2025.

Kwa mujibu wa Mahakama, mshitakiwa ametiwa hatiani na amehukumiwa kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini.

NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
Rais Ruto kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5
Rais Ruto kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5
UDASA waichambua hotuba ya Jaji Chande
UDASA waichambua hotuba ya Jaji Chande

News Analysis

RC Singida apongeza jitihada za NBC kuchochea kasi ya mapinduzi ya kilimo
RC Singida apongeza jitihada za NBC kuchochea kasi ya mapinduzi ya kilimo

 

MKUU wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amepongeza mchango wa wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo huku akiitaja kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” kuwa nyenzo muhimu ya kuimarisha ustawi wa wakulima na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika jana Singida, Dendego alisema ujio wa mpango huo kwa mara ya kwanza mkoani humo ni hatua muhimu inayochochea utekelezaji wa malengo ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati na kuinua kipato cha wakulima.

Hafla hiyo iliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika, wakulima, pamoja na washiriki wengine katika mnyororo wa thamani wa kilimo. Uongozi wa NBC katika uzinduzi huo uliwakilishwa na Mkuu wa Idara ya Bima, Benjamini Nkaka, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima, Raymond Urassa, wakiongoza timu ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kanda ya Kati, Miraji Msuya.

Kwa mujibu wa Dendego, ujio wa kampeni hiyo unaenda sambamba na jitihada za Serikali ambazo tayari zimeanza kuzaa matunda, ikiwemo usajili wa zaidi ya asilimia 92 ya wakulima mkoani Singida, utoaji wa ruzuku za pembejeo kama mbegu na mbolea, pamoja na uwekezaji katika huduma za ugani na kilimo cha umwagiliaji.

“Kampeni ya NBC Shambani inakuja kuimarisha juhudi hizi kwa kuchochea ujumuishaji wa kifedha kwa wakulima. Hii ni hatua muhimu kuelekea kilimo chenye tija na chenye manufaa kwa wananchi mmoja mmoja, kaya na mkoa kwa ujumla,” alisisitiza.

Aidha, RC Dendego aliwahimiza wakulima kuchangamkia fursa zinazotolewa na kampeni hiyo, akitaja baadhi ya manufaa yake kuwa ni pamoja na akaunti zisizo na makato ya kila mwezi, upatikanaji wa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo, elimu ya fedha, pamoja na huduma za bima ya afya na mazao.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni hiyo, Nkaka alisema NBC inaendelea kubuni suluhisho bunifu za kifedha ili kuunga mkono azma ya Serikali ya kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030. Alibainisha kuwa benki hiyo imejikita pia katika utoaji wa elimu ya fedha, huduma za kidijitali, pamoja na bima zinazolenga kupunguza hatari kwa wakulima.

Kwa upande wake, Urassa alisema kampeni hiyo ya miezo minne, inalenga wakulima wa mazao ya dengu, choroko, mbaazi, soya na ufuta, na inatoa fursa kwa wakulima binafsi pamoja na kupitia vyama vya ushirika kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali, ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato (laptops).

“Lengo kuu ni kuwahamasisha wakulima kutumia mifumo rasmi ya kifedha kwa kutunza fedha zao benki. Tunawakaribisha kufungua akaunti za NBC Shambani ili waweze kunufaika na huduma na fursa hizi,” alieleza.

Baadhi ya wakulima walioshiriki uzinduzi huo walieleza matumaini yao juu ya kampeni hiyo, wakihimiza wenzao kuitumia vyema ili kunufaika na fursa za kifedha, elimu, bima na zawadi zinazotolewa.

NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
NBC yaitambulisha “NBC Shambani” kwa wakulima wa Songwe
Meridianbet na uwekezaji wa utu kwa wagonjwa Mwananyamala
Meridianbet na uwekezaji wa utu kwa wagonjwa Mwananyamala
EACOP yaweka rekodi ya saa milioni 6 bila ajali kazini
EACOP yaweka rekodi ya saa milioni 6 bila ajali kazini

Latest News

error: Content is protected !!