RAIS wa Kenya, William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zinajadili mpango wa kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga, kikifanana na kile cha Aliko Dangote cha nchini Nigeria.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Ruto amebainisha kuwa kiwanda hicho kitahudumia nchi kadhaa kwa kutumia mafuta ghafi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini na Uganda.
Kwa upande wake Dangote amesema yuko tayari kujenga kiwanda kama chake chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku, ikiwa serikali za nchi hizo zitatoa ushirikiano.
ZINAZOFANANA
Askari aliyemkamata Rais wa Venezuela akamatwa
Haki isiwe chombo cha kutolea adhabu pekee-Papa Leo
Marekani itaendelea kuweka kizuizi cha kijeshi Hormuz-Trump